Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Spaletti ashinda Tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka Serie A

Luciano Spaletti Napoli Lucianoa Spaletti

Fri, 2 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Luciano Spalletti ameteuliwa kuwa Kocha Bora wa Serie A wa Msimu baada ya kuiongoza Napoli kutwaa taji lao la kwanza la Scudetto katika kipindi cha miaka 33, na la kwanza katika taaluma yake pia.

Mtaalamu huyo atapokea kombe wakati wa kujiandaa na mchezo wa mwisho wa msimu wa Napoli dhidi ya Sampdoria kwenye Uwanja wa Stadio Diego Armando Maradona wikendi hii.

Tuzo hiyo ilipigiwa kura na wahariri kutoka vyombo vya habari vya michezo vya Italia, wakichagua mgombea wao kwa kuzingatia sio tu matokeo na ubora wa mpira wa miguu, lakini pia tabia ya uchezaji wa haki wakati wa mechi.

Mkuu wa Lega Serie A, Luigi De Siervo amesema; “Msimu wa Luciano Spalletti kuinoa Napoli umekuwa wa ajabu. The Azzurri walifanya alama yao kutoka siku ya kwanza sio tu kwa matokeo yao, lakini pia mtindo wa kuvutia wa kandanda, ambao ulithaminiwa sana katika kiwango cha kimataifa.”

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 64 ameamua kuwa anataka kuchukua mapumziko baada ya ushindi wa Scudetto, hivyo Napoli wanahitaji kutafuta kocha mpya wa kuwaongoza katika kampeni za 2023-24.

Hii ilikuwa Scudetto yake ya kwanza na Spalletti alichora tattoo kwenye mkono wake kuwakilisha ushindi.

Tayari alitajwa kuwa Kocha Bora wa Serie A katika misimu yote ya 2004-05 na 2005-06.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: