Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida wataendeleza uteja mbele ya Simba SC leo?

Simba Vs Singida FG Singida wataendeleza uteja mbele ya Simba SC leo?

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uhondo wa kombe la Mapinduzi 2024 unazidi kukolea utamu leo Januari 10, 2024 ambapo utapigwa mchezo wa kuhitimisha hatua ya nusu fainali huku Singida Fontaine Gate FC ikiangazia kulipa kisasi cha kufungwa 2-0 na Simba SC kwenye hatua ya makundi.

Singida Fontaine Gate FC imetinga nusu baada ya kuwaondosha Wanalambalamba Azam FC katika ushindi wa 2-1 kwenye robo fainali huku Simba SC ikifika hatua hiyo kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Jamhuri SC.

Singida Fontaine Gate FC na Simba SC zimekutana mara tatu ndani ya miezi mitano iliyopita ambapo Simba SC imeibuka kidedea mara zote tatu.

Ushindi wa penalti 4-2 kwa Simba Sc kwenye nusu fainali ya Ngao ya Jamii 2023, ushindi wa 2-1 kwenye mchezo wa Ligi kuu na ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya #MapinduziCup2024

Je Wakulima wa Alizeti wataendeleza uteja mbele ya Mnyama?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: