Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yawaruhusu mastaa wake kujiunga kambi ya Stars

Mastaa Simba SC Kambini Simba yawaruhusu mastaa wake kujiunga kambi ya Stars

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wachezaji wa Simba Kibu Denis na Mzamiru Yassin wameonakena kwenye mazoezi ya kikosi cha timu ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars' kinachojiandaa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Sudan.

Mechi hiyo itapigwa nchini Saudi Arabia na mastaa tayari washaingia kambini kujiandaa na mechi hiyo.

Wakati mechi hiyo ikipigwa nchini humo Simba SC imebakiza siku saba kutoka leo kucheza mechi ya ufunguzi ya African Football League dhidi ya Al Ahly katika uwanja wa Mkapa jijini Dar (Oktoba 20) huku wapinzani wao Al Ahly tayari washatoa taarifa ya kuwazuia mastaa wake wakiwemo Percy Tau kujiunga kikosini Afrika Kusini na Aliou Dieng kwenda Mali.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: