Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yawafuata Wydad kibabe

Simba Ngf.jpeg Simba yawafuata Wydad kibabe

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Simba SC kimeondoka leo jioni kwenda Morocco kwa ajili ya mchezo wa marudiano na wenyeji, Wydad Club Athletic Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Ijumaa Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca.

Tayari Kikosi hicho kimefika Dubai na safari itaendelea itakapofika saa 1:45 asubuhi kuelekea jijini Casablanca Morocco kuifuata Wydad Athletic Club kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika usiku wa Ijumaa ya Aprili 28, 2023.

Simba inahitaji sare kwenda Nusu Fainali baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa hao watetezi Jumamosi, bao pekee la mshambuliaji Mkongo, Jean Othos Baleke dakika ya 30 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Wakati Wydad ina mataji matatu ya CAF Champions League (1992, 2017 na 2021–22), mafaniko makubwa kwa Simba kwenye michuano hiyo ni kufika Nusu Fainali mwaka 1974 ilipoitoa Hearst Of Oak ya Ghana kwa mabao 2-1 kabla ya kutolewa na Ghazl El Mahalla yenye maskani yake mji wa El Mahalla El Kubra kwa penalti 3-0 kufuatia sare ya jumla ya 1-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: