Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yamvutia waya jezi namba sita wa Yanga

Mohamed Zougrana 6.jpeg Mohamed Zougrana

Thu, 6 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati Yanga wakitamba Dar es Salaam kwamba kuna kitu jezi namba 6 kinatua kushtua nchi,imevuja kwamba hawajamalizana na mido jezi namba 6 wa Asec, Mohamed Zougrana ambaye Simba wamemwekea mkataba mezani

Afisa Habari wa Yanga Ally Kamwe juzi katika mkutano na waandishi wa habari alisema wameshamaliza usajili na wataanza kutambulisha wachezaji na jezi namba sita atakuwa wa mwisho kutambulishwa

"Kwa asilimia 100 usajili wa Yanga umeshafungwa wachezaji wote ambao tulikuwa tunawahitaji kwa ajili ya kwenda kuboresha benchi la ufundi kwa mujibu wa pendekezo la mwalimu wote tayari uongozi wameshamalizana nao kwa mikataba yao na wameshasaini"

" Tunasubiri zoezi la utambulisha jezi umalizike kama itakuwa katiki ya wiki kwahiyo wiki hii haitafika mwisho tutaanza kushuisha vyuma, kuhusu jezi namba sita na mmeshindwa kumjua atakae vaa jezi namba sita Yanga msimu ujaio"

" Tayari usajili wetu umeshafungwa tunasubiri kuwatambulisha wachezaji"

Zougrana ambaye alionyesha uwezo wa juu kwenye michuano ya Caf msimu uliopita amekuwa akihusishwa kujiunga na Yanga ingawa mabosi wa timu hiyo bado hawajaweka wazi hatua za usajili huo lakini Wekundu hao wako naye mezani kuanzia wikiendi iliyopita wakipambana naye.

Zougrana ni kiungo aliyepiga kazi kubwa kwenye eneo la kati la ASEC wakiiishia nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika akiwa na ubora wa kupiga pasi na hata kufunga.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: