Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yamfuata kiungo Zambia, Saido bye bye

Saido Bye Bye Simba yamfuata kiungo Zambia, Saido bye bye

Sat, 15 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mwanaspoti linafahamu Simba imefikia pazuri na winga wa Power Dynamos ya Zambia, Joshua Mutale (22) na sasa ipo hatua ya mwisho kumalizana na uongozi wa timu yake na wanafikiria kumpa mkataba wa miaka miwili.

Habari za ndani ni kwamba ujio Mutale ndani ya kikosi hicho ni kuchukua nafasi ya Mrundi Said Ntibazonkiza’Saido’ ambaye muda wowote anaweza kupewa mkono wa kwaheri Msimbazi.

Winga huyo msimu uliopita katika mechi 26, alifunga mabao matano, asisti tatu na dakika 453.

Anayesimamia usajili huo ni Crescentius Magori ambaye ni miongoni mwa vigogo walioongezwa kwenye jopo jipya la usajili wa Simba chini ya Muwekezaji Mohammed Dewji ‘Mo’.

Habari zinasema kwamba asilimia kubwa dili hilo linaendelea vizuri na uwezekano wa staa huyo kutua Msimbazi ni mkubwa.

“Kipengele kilichosalia ni kumalizana na uongozi wa timu ya Power Dynamos, naamini hatutashindwana nao, hivyo hadi sasa kwa asilimia kubwa, mchezaji huyo atakuwa sehemu ya kikosi cha Simba msimu ujao,”alidokeza kigogo mmoja ndani ya Simba.

Inaelezwa kuwa Magori tayari yupo Zambia, alionekana Uwanja wa Levy Mwanawasa, mjini Ndola ambapo Stars ilikuwa inacheza dhidi ya taifa ya Zambia, mechi ya kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2026,ikiwa kundi E.

Simba iliwahi kumfuata winga huyo, katika usajili wa dirisha dogo, lakini mambo hayakwenda vizuri, ikishindikana kuwa sehemu ya kikosi hicho.

“Ni mchezaji mzuri sana, ndio maana alikuwa anafuatiliwa kwa muda mrefu, ukiachana na Mutale Simba inasajili kikosi ambacho kitakuwa na ushindani mkubwa na kurejesha furaha ya mashabiki, kutokana na kukosa ubingwa misimu mitatu mfululizo,” alisema.

MO amepania kuifumua Simba na amekiri kwamba anatamani msimu ujao ladha yao ya soka Biriani ionekane Uwanjani kwani wameyumba vya kutosha. Tayari Dewji, amezuia uwezekano wa beki Joyce Lomalisa kutua Msimbazi lakini amemuita kipa Ayoub Lakred kwa ajili ya mazungumzo nyumbani kwake nchini Dubai.

Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti inazo ni kwamba Ayoub ambaye mkataba wake na Simba imemalizika amewaambia viongozi wa Simba kwamba ana ofa mbili kutoka klabu ya Pyramids na Zamalek zote za Misri. Lakini Mo akawaambia kwamba atapambana kuhakikisha anabaki.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: