Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yalazimishwa sare Uturuki

Kibu Denis Prosper Mfungaji wa bao la Simba

Mon, 24 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba leo Julai 24 imecheza mechi ya kwanza ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Zira FC inayoshiriki Ligi Kuu Azerbaijani kwenye uwanja wa Voneesortna uliopo mjini Bolu, Uturuki.

Mechi hiyo imemalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 huku bao la Simba limefunga kupitia kwa Kibu Denis akimalizia pasi ya Saido Ntibazonkiza kipindi cha kwanza.

Bao la kusawazisha la Zira limefungwa na Rustam Ahmadzade akisawazisha dakika ya 63.

Simba inaendelea na kambi yake nchini Uturuki kujiandaa na msimu wa 2023 itakaposhiriki michuano ya ndani na ya kimataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: