Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yakubali kichapo Cairo, yatolewa tena Robo Fainali CAF

Al Ahly Vs Simba 2 0.jpeg Simba yakubali kichapo Cairo, yatolewa tena Robo Fainali CAF

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Simba SC kwa mara nyingine imetupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika Hatua ya Robó Fainali baada ya kufungwa 2-0 na wenyeji, Al Ahly usiku huu Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo nchini Misri.

Mabao yaliyoizamisha Simba leo yamefungwa na kiungo mzawa, Amr El Soleya dakika ya 47 akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji Mfaransa, Anthony Mbu Agogo Modeste na mshambuliaji mzawa, Mahmoud Abdelhamid Soliman dakika ya 90na ushei.

Kwa matokeo hayo Al Ahly inakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 3-0 kufuatia kushinda 1-0 pia kwenye mchezo wa kwanza Ijumaa iliyopita Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Sasa Mabingwa hao watetezi, Al Ahly na watamenyana na mshindi kati ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Petro de Luanda ya Angola katika Nusu Fainali, ambao mechi ya kwanza zilitoka sare ya 0-0 Jijini Lubumbashi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: