Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaja na hii ya 'Kwanza Tanzania'

Ahmed Ally Ms Simba yaja na hii ya 'Kwanza Tanzania'

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba imezindua channel mpya kupitia mtandao wa WhatsApp na imetambulishwa na CEO wa Klabu hiyo, Imani Kajula kwa ajili ya kuwaweka pamoja mashabiki na kurahisisha upatikanaji wa taarifa rasmi za klabu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema;

"Katika maeneo yote ya mitandao ya kijamii Simba tumekuwa tukifanya vizuri na leo tunakwenda kuzindua mtandao mwingine na itakuwa na faida kwa namna gani kwa mashabiki.

"Tunafahamu urahisi wa kutumia WhatsApp kwa hiyo hii itakuwa njia rahisi ya kufikia watu wengi. Kuna wengine hawatumii Instagram wala Facebook lakini wana WhatsApp," amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: