Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaipiga za uso Yanga, yabeba watatu

Ahmed Ally Wiki Ya Thank You Simba yaipiga za uso Yanga, yabeba watatu

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Klabui ya Simba umeeleza kuwa ukimya wao una kishindo baada ya watu maalum kuingia sokoni kufanya usajili.

Simba wanataka kuepuka makosa waliyofanya misimu iliyopita kwa kuweka wary makini kwenye usajili.

Imeelezwa kuwa Simba tayari imemalizana na nyota watatu wapya akiwemo Yusuph Kagoma (Singida Fountain Gate FC) ambaye pia alikuwa akihusishwa kutua Yanga, Lameck Lawi (Coastal Union) na Elie Mpanzu (AS Vita Club) ya DR Congo.

Akizungumza nasi, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema tangu ligi imalizike wamekuwa kimya hali ambayo imeleta hofu kwa mashabiki wao .

Amesema usahihi ni kuwa mpango na mipango thabiti inaendelea na itakapokuwa tayari wanasimba watafahamu juu ya ukimya waliokuwa nao kwa kipindi chote.

“Jambo la kufurahisha ni kwamba mipango yote inatekelezwa kwa ustadi na ufanisi wa hali ya juu mno, malengo tuliyoiweka ya kuboresha timu yetu yamefanikiwa kwa asilimia kubwa kwa maana mipango yetu kwenye soko la usajili iko vizuri.

“Niwaombe wanasimba tutulie, tutafurahi kila kitu kuhusu timu yetu kinaenda sawa, ikiwemo suala la usajili haturudii makosa yaliyojitokeza awali,” amesema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: