Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaingia makubaliano na ATCL

F7 XIRHWYAAqfJW.jpeg Simba yaingia makubaliano na ATCL

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) leo zimekubaliana kuendelea kushirikiana na kuipa klabu hiyo fursa ya kutumia huduma za Kampuni ya ATCL.

Akizungumza baada ya kufanya ziara ya kuishukuru ATCL kwa uhusiano mzuri na Simba, Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba Imani Kajula alisema, "ATCL Mmekuwa washirika muhimu sana kwenye mafanikio ya Klabu ya Simba kwa kutupa usafiri wa uhakika na bora kwa ajili ya timu yetu. Tukielekea kwenye mechi ya AFL dhidi ya Al-Ahly tufurahi kujua kwamba ATCL itakuwa mbia muhimu kusafirisha mashabiki kutoka sehemu mbalimbali kuja kuangalia mchezo huo."

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ATCL Jamal Athumani Kiggundu alisema, "ATCL inafurahi sana kuwa mbia wa Simba na iko tayari kufanya kazi pamoja na Simba katika kusafirisha timu na pia mashabiki."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: