Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yafunguka sababu ya kumupiga bei Inonga

Inonga Sz Sad Simba yafunguka sababu ya kumupiga bei Inonga

Tue, 25 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya kumuuza mlinzi wa kati, Henock Inonga Baka kwenda FA Rabat inayoshiriki Ligi Kuu nchini Morocco.

Akiuzngumzia hilo, Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema kutokana na klabu kujali maslahi ya wachezaji, wamemruhusu beki huyo kuondoka kwenda kujiunga na FA Rabat.

“Taarifa ambayo napenda kuitoa kwa sasa ni kwamba tumeachana rasmi ama tumemuuza beki wetu wa kati Henock Inonga Baka kwa Klabu ya AS FAR Rabat ya Morocco na kuanzia sasa Inonga ni mchezaji halali wa FAR Rabat.

“Simba tumemuuza Inonga akajaribu bahati yake kunako nchi ya Morocco. Huo umekuwa utaratibu wetu mchezaji anapotakiwa na Klabu kubwa zaidi, sisi huwa tunafanya biashara na hasa mchezaji anapoonesha nia ya kutaka kuondoka. Sisi sio kama wale wanaong’ang’ania mchezaji kama ndoa.

“Mkataba wa Inonga ulikuwa unamalizika mwaka 2025 lakini kwa maslahi mapana ya klabu na mchezaji mwenyewe, tumeamua kumpiga bei akajaribu maisha mengine mapya,” amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: