Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yadondosha alama Chamazi, Wazir Jr avuruga Shughuli

Kmc Vs Simba 2 2 Mchezo umemalizika kwa sare ya mabao 2-2

Sat, 23 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dakika 90 za mtanange wa kukata na shoka zinamalizika katika Uwanja wa Azam Complex huku mnyama Simba SC akidondosha alama mbili kufuatia sare 2-2 dhidi ya "Kino Boys".

KMC ndio waliokuwa wa Kwanza kupata bao kupitia kwa Waziri Jr 32’ Bao ambalo lilidumu mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika.

Kipindi cha Pili Simba walirudi kwa Kasi na hatimaye dakika ya 57 Ntibanzokiza (P) akaisawazishia Simba kwa bao la mkwaju wa Penati na kisha Baleke akaongeza la pili dakika ya 58’.

Alikuwa ni yuleyule Waziri Jr ambae dakika ya 88 anawapa KMC bao la kusawazisha na kufanya matokeo kuwa 2-2.

Kwa Matokeo hayo, Simba inasalia nafasi ya tatu alama 23 baada ya mechi 10 huku KMC FC ikikwea mpaka nafasi ya nne alama 21 baada ya mechi 14.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: