Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba ya Benchikha, tutarajie pira biriani?

Benchikha Simba Ms Simba ya Benchikha, tutarajie pira biriani?

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hakuna asiyefahamu kuwa mjini ameshuka Kocha wa kazi kweli, huyu ni ‘show show’, ukibisha kawaulize Yanga kwenye Fainali ya Kombe la Shirikisho msimu uliopita, mwamba alibeba ubingwa akiwa anatabasamu, Nabi akinywa maji muda wote kushusha presha.

Simba tunaweza kusema hapa wamelamba karata dume. Licha ya ubora wa Kocha Benchikha na benchi lake la Ufundi lakini kama hatakuwa na Mazingira rafiki, Ushirikiano kutoka kwa mabosi zake na Wachezaji basi itakuwa kazi bure hata angeshuka Pep Guardiola.

Ni wakati sasa wa Klabu ya Simba kumaliza tofauti zao kuanzia Mashabiki, Wachezaji mpaka Uongozi ili kumrahisishia kazi ‘Kocha la Boli’.

Profile ya Kocha ni kubwa mno jambo ambalo haikuwa rahisi kwa watu kuamini kuwa Benchikha angekuja kuifundisha Simba, lakini imewezekana.

Mashabiki wa Simba wamekuwa wakisikika wakilalama kuwa walikuwa wakipata matokeo lakini soka walilokuwa wakicheza wachezaji wao si la kuvutia. Ikafika wakati hata hayo matokeo kwa 'pira kokoto' yakawa magumu, Robertinho mzee wa Objective Football wakamsepesha.

Simba wamezoeleka kucheza mchezo wa pasi nyingi na kushambulia kwa kasi kupitia viungo hasa wa kati, lakini hivi karibuni watani zao Yanga ndiyo wametawala staili hiyo ya soka hapa nchini.

Simba wanataka kuurudisha ufalme wao wa kuchezea soka ambao wameupoteza kwa miaka kadhaa sasa, kwa Benchikha itawezekana?

Je, Simba SC ya Benchikha unaitabiria kitu gani?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: