Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wakijisahau tu, Mzamiru anasepa

Kiungo Punda Mzamiru Kiungo wa Simba, Mzamiru Yassin

Wed, 8 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Simba ikiwa kwenye mapambano ya kuhakikisha Kibu Denis anasaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Msimbazi, kuna tetesi kuwa Mzamiru Yassin yupo kwenye mawindo ya Ihefu na Azam FC.

Inatajwa kuwa tayari Ihefu imewasilisha ofa mezani kwa Mzamiru huku Azam FC ikiwa imeonesha nia ya kutaka kumsajili kiungo huyo ambaye amedumu Simba kwa muda mrefu tangu aliposajiliwa akitokea Mtibwa Sugar.

Mkataba wa Mzamiru na Simba unamalizika mwishoni mwa msimu lakini hadi sasa bado hajaongeza mkataba mwingine, kwa hiyo kama Simba haitamuongezea mkataba mpya huenda akaondoka akiwa mchezaji huru.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: