Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba waja na kubwa kuliko kwa Mashabiki

CEO Simba SC, Iman Kajula.jpeg Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba leo imezindua shindano la MFALME SHANGWE kwa ajili ya mashabiki, kupitia shindano hilo mashabiki wataweza kujishindia zawadi mbalimbali baadhi ya zawadi hizoni tiketi za mechi pamoja na fedha taslimu ambazo jumla yake ni Tsh. 500 milioni.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula amesema MFALME SHANGWE inaunganishwa na maendeleo ya timu kwa ushabiki wenye faida na miongoni mwa eneo ambalo litafaidika na mapato ambayo yatapatikana kupitia MFALME SHANGWE ni eneo la timu ya vijana.

“Tunawakaribisha wanasimba na mashabiki wa soka Tanzania kushiriki MFALME BINGWA, tunaamini tutaendelea kujitahidi ili Simba iwe sehemu ya furaha yenu kuelekea mwisho wa mwaka huu.”

Moja ya wajibu mkubwa wa shabiki wa Simba ni kuisaidia timu yao kwa kununua bidhaa za klabu. Unaponunua bidhaa za klabu unasaidia klabu kujijenga kwenye mifumo ya kifedha. Ni wazi kwamba uendeshaji klabu ni gharama kubwa sana.

Klabu ya Simba inataka kuwafanya mashabiki wake kuwa sehemu ya kuchangia mafanikio ya timu lakini wakati huohuo wakijishindia zawadi mbalimbali wakati huu kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: