Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wabanwa mbavu Zambia, Chama aokoa jahazi

F6J38egXkAApzzW.jpeg Simba wabanwa mbavu Zambia, Chama aokoa jahazi

Sat, 16 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi Simba SC wana kibarua cha kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo wa mkondo wa pili dhidi ya Power Dynamos baada ya leo kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Power Dynamos.

Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Levy Mwanawasa nchini Zambia uliwashuhudia wawakilishi hao wa Tanzania wakitoka nyuma mara mbili na kulazimisha sare hiyo.

Mabao ya Power Dynamos katika mchezo wa leo yamefungwa na Lakred akijifunga 29 na Mulombwa C. 75.

Mabao ya kusawazisha ya Simba yamefungwa na kiungo wa Kimataifa wa Zambia Clatous Chama.

Mchezo wa mkondo wa pili utapigwa Oktoba 1 Jijini Dar es Salaam ambapo Simba atakuwa mwenyeji.

Kwa kiwango kilichooneshwa na Simba unadhani atachomoka mbele ya Power Dynamos mchezo wa marudiano? Tupe maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: