Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba vs Power Dynamos, huyu ndie wa kumchunga

Simba Chunga Simba vs Power Dynamos, huyu ndie wa kumchunga

Sun, 1 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wengi waki wakimtazama Joshua Muthale kuwa ndiye mchezaji hatari kwenye kikosi cha Power Dynamos siku ya Leo.

Lakini niwaeleze tu watu wa Mpira kuwa mtu mwingine hatari na wa kuchungwa ni mshambuliaji wa kati raia wa Congo DR Andy Boyeli.

Boyeli hadi hivi sasa takwimu zake ni hizi.

Msimu wa 2023/24 Ligi kuu Zambia amecheza mechi tatu (3) amefunga goli moja (1).

Msimu wa 2022/23 Ligi kuu Zambia amecheza mechi 12 na kufunga goli 11 na assist tatu (3).

Katika michezo 27 aliyocheza kwenye Ligi kuu soka Zambia amefunga magoli 19 na Assist tatu (3).

Huyu ni mshambuliaji wa kuchungwa zaidi leo, nafasi moja tu ana kuadhibu na hata kule Zambia aliwasumbua sana mabeki wa Simba,

Mtihani Mkubwa kwa Simba Sc ni kukosekana kwa Henock Inonga Leo licha ya kuwa tunajua Robertinho amekiandaa kikosi hicho ila inatakiwa kazi kubwa na ya Ziada Leo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: