Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba vs Namungo haijawahi kuwa rahisi

Ally Salim X Lakred Simba vs Namungo haijawahi kuwa rahisi

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kitaumana leo kwa wababe wawili ndani ya uwanja kusaka pointi tatu muhimu kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru.

Ni Simba watakuwa nyumbani wakiikaribisha Namungo wauaji wa kusini kwenye mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na haitakuwa kazi rahisi kwa wote jasho litamwagika.

Hapa tunakuletea baadhi ya hesabu zitakazoongeza ugumu kwa timu zote mbili namna hii:-

Ngoma ni nzito Msimu wa 2022/23 kwenye msako wa pointi sita, ni nne zilikuwa kwa Simba na moja ilikuwa ni mali ya Namungo. Kwenye mchezo wa kwanza Simba ilishinda na ule wa pili ngoma ilikuwa sare ya kufungana bao 1-1.

Mchezo wa kwanza ilikuwa ni Novemba 16 2022 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 1-0 Namungo na mzunguko wa pili Mei 3 2023 ubao wa Uwanja wa Majaliwa ulisoma Namungo 1-1 Simba.

Ally Salim anakumbuka namna alivyokuwa kwenye harakati zake za kuokoa mpira wa pigo la kona uliomshinda na kuzama mazima ndani ya 18.

Makocha wakuu wote wamesanda Timu zote mbili zinakutana zikiwa na sura mpya kwenye benchi la ufundi baada ya makocha waliokuwa kwenye timu hizo kusanda. Roberto Oliveira alikuwa ndani ya kikosi cha Simba alifikia makubaliano ya kusitisha mkataba wake na mabosi wa timu hiyo.

Oktoba alikomba tuzo ya kocha bora, Novemba 5 alikuwa shuhuda ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 1-5 Yanga. Novemba 7 mkataba wake ulisitishwa na sasa timu ipo mikononi mwa Daniel Cadena aliyekuwa kocha wa makipa akishirikiana na Seleman Matola.

Picha ipo hivyo kwa Namungo pia Cedrick Kaze aliyekuwa kocha mkuu mwanzo wa msimu alibwaga manyanga. Ilikuwa ni Oktoba 22 2023 kutokana na kutokuwa na mwendo mzuri katika kikosi hicho.

Timu ya Namungo ipo mikononi mwa Dennis Kitambi ambaye alikiongoza kikosi hicho kupata ushindi wa kwanza mbele ya Azam FC. Ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Azam FC 1-3 Namungo ilikuwa ni Novemba 27.

Wametoka kugumu wote Wapinzani hawa wawili wote wametoka kwenye dakika 90 ngumu kwa kukwama kuambulia pointi tatu kwenye mechi zao. Wenyeji Simba hawa ilikuwa ni majanga kwao walipoteza pointi tatu mazima dhidi ya Yanga.

Namungo Novemba Mosi waliambulia pointi moja Uwanja wa Mkwakwani ubao uliposoma Coastal Union 0-0 Namungo.

Ukuta ni tatizo Ukuta wa timu zote mbili haupo imara kutokana na kuokota mabao mengi kwenye mechi walizocheza. Ule wa Simba unaoongozwa na Henock Inonga katika mechi 7 umeokota jumla ya mabao 10.

Ule wa Namungo wenye kiraka Erasto Nyoni kwenye mechi 8 umeokota jumla ya mabao 8 ikiwa na wastani wa kuokota bao moja kwenye kila mchezo.

Vita ya nafasi Ni mwendelezo wa mzunguko wa kwanza ambapo timu zote zinasaka kuwa ndani ya tatu bora. Simba pointi tatu ikikomba leo itazidi kujiimarisha ndani ya tatu bora kwa kuwa ina pointi 18.

Namungo wao wakikomba pointi tatu wataanza kuiwinda 10 bora kwa kuwa pointi zao walizonazo zinawapa nguvu kuwa nafasi ya 12 na pointi 7.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: