Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba tunashinda nje ya uwanja ila uwanjani ni wabovu - Mchome

Simba Rekodi CAF.jpeg Simba tunashinda nje ya uwanja ila uwanjani ni wabovu - Mchome

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki kindakindaki wa Simba SC, Mchome Mapovu amesema kuwa timu hiyo kimataifa inashinda nje ya uwanja lakini ni wabovu uwanjani.

Mchome amesema hayo baada ya Simba kukubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Tanzania Prisons juzi katika uwanja wa CCM Jamhuri mjini Morogoro.

“Simba ya mashindano ya kimataifa tunashinda nje ya uwanja. Ndio maana tukija kwenye ligi wanatujua kila kitu, kutudhibiti inakuwa rahisi. Simba ukija uwanjani ni wabovu mno.

“Ndio maana kocha wa Galaxy alilalamika walikuwa wanatapika hovyo, unaweza kusema ni kweli. Haiwezekanai unamuua mtu bao 6-0 halafu unakuja kufungwa na Prisons ambayo yuko nafasi ya sita huko, anakufunga na wewe unasema unataka ubingwa, tubadilike,” amesema Mchome.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: