Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba sasa ni ‘full’ mkoko

Simba SC BB.jpeg Kikosi cha Simba SC

Thu, 25 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi chote cha wachezaji wa Simba ambao hawajaitwa kwenye timu zao za taifa leo kinaanza kujifua tayari kwa ajili ya kujiweka sawa na ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), huku Belhack Benchikha akisema: “Nawatakawote mazoezini.”

Simba imewapa mapumziko ya siku 10 mastaa wa timu hiyo baada yakutoka kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024, iliyofika fainali na kufungwa bao 1-0 na Mlandege.

Ni Aishi Manula, Mzamiru Yassin, Kibu Denis, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Clatous Chama pekee ambao watakosekana kwenye mazoezi hayo kutokana na kuwa kwenye vikosi vya timu zao za taifa zinazoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 Ivory Coast.

Benchikha ambaye nikocha mkuu wa Simba, ameuambia uongozi wa timu hiyo kuwa hataki visingizio kutoka kwa mchezaji yeyote, bali anataka wote ambao hawana majukumu ya mataifa yao kuwahi kambini haraka.

“Nawahitaji wachezaji wote mazoezini sitarajii visingizio kutoka kwa mchezaji yeyote kwani tayari nimefanya jitihada za kuzungumza na mchezaji mmoja mmoja kwa ajili ya kumkumbusha hilo,” alisema kocha huyo ambaye pia hayupo nchini lakini amelithibitishia gazeti hili kuwa atatua muda wowote kuanzia sasa.

“Hivyo natarajia kukutana na wachezaji wangu wote tayari kwaajili ya kujiweka sawa na michuano yote iliyo mbele yetu.”

Wakati kocha akifunguka hayo staa mpya wa kikosi cha Simba, kiungo Babacar Sarr ambaye tayari amepata dakika za kucheza ndani ya timu hiyo kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024, alisema hayupo nchini lakini atawasili muda wowote tayari kwa ajili ya maandalizi.

“Ni kweli baada yakupewa mapumziko nilirudi nyumbani, lakini natarajia kuja Tanzania muda wowote tayari kwa ajili ya kujiweka fiti kwa mashindano kama kocha alivyotuagiza,” alisema.

Mastaa wengine wapya waliosajiliwa na Simba ni viungo washambuliaji Saleh Karabaka kutoka JKU na Ladack Chasambi (Mtibwa Sugar) pamoja na mastraika wawili Mgambia Pa Omar Jobe na Muivory Coast Freddy Michael Kouablan aliyeongoza kwa ufungaji mabao katika Ligi Kuu Zambia akifunga mabao 14 na asisti nne katika mechi 16 alizocheza.

Hata hivyo, mashabiki wa Simba wanasubiri kwa hamu kubwa kuwaona Freddy na Jobe ambao bado hawajaonyesha makali Tanzania, tofauti na Sarr aliyeonekana kwenye Mapinduzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: