Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba na bajeti ya matuamini

Try Again Hj Simba na bajeti ya matuamini

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba imetangaza bajeti ya Sh 25 bilioni kwa msimu wa 2023/2024 ikiwa ni ongezeko la Sh10 bilioni kutoka bajeti yao ya msimu uliopita ambayo ilikuwa ni Sh15 bilioni.

Hayo yamesemwa jana katika mkutano mkuu wa mwaka wa klabu hiyo uliofanyika katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Julius Nyerere Dar es Salaam.

Mhasibu wa Simba, Suleiman Kahumbu alisema kuwa bajeti hiyo ya msimu huu inategemea zaidi vyanzo mbalimbali vya mapato vya klabu hiyo kama vile udhamini na viingilio.

 "Matumizi ya 2022/23 yalipangwa kuwa Tsh. 12,363,626,983 lakini matumizi halisi ni Sh 15,936,829,943. Bajeti kwa mwaka 2023/2024 klabu imepanga kukusanya kiasi cha Sh 25,930,722,300 lakini imepanga kutumia kiasi cha Sh 25,423,997,354. Tutabaki na mapato ya ziada ya Sh 506,724,946."

“Aidha mapato yote hayo yanapatikana kutokana na vyanzo mbalimbali vya mapato ndani ya timu kama fedha ya mdhamini,haki za matangazo,mapato ya Mlangoni,uuzwaji wa jezi, wadhamini wadogo wadogo na kushiriki katika michuano ya AFL jambo ambalo limechangia kwa asilimia kubwa kuweza kupata mapato makubwa kwa klabu yetu msimu huu,"  alisema Kahumbu.

Kahumbu alisema kuwa mwekezaji na Rais wa heshima wa Simba, Mohammed Dewji 'MO' amekuwa akitoa mchango mkubwa katika bajeti ya klabu hiyo na mfano ni msimu uliopita ambapo alichanga kiasi cha Sh 2.4 bilioni.

Katika hatua nyingine, wanachama wa klabu hiyo wamepitisha maboresho ya baadhi ya vipengele vya katiba yao ili kutimiza matakwa na maelekezo ya serikali.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maboresho ya Katiba ya klabu ya Simba, Hussein Kitta amesema wanachama wamepitisha mambo sita ambayo walitakiwa kufanyia maboresho huku suala la uwakilishi wa wanachama kwenye mkutano mkuu likigonga mwamba.

Alisema katika mambo hayo wanachama wamekataa kupitisha kipengele kimoja kinachoeleza kila tawi kutoa wawakilishi wachache kwenda katika mkutano mkuu.

"Hicho kipengele tuliambiwa tukiweke kulingana na namna ya kuendesha mikutano yetu, lakini wanachama wamekikataa, kutokana na hilo ni sehemu ya mapendekezo tu tuliopewa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT ) ambayo haikuwa na ulazima," alisema Kitta.

Mwakilishi wa mgeni rasmi, Nicolas Mihayo akimwakilisha Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), alisema anawapongeza  Simba kwa kufuata maelekezo ambayo ilipewa kufanyia kazi katika mapendekezo ya marekebisho ya katiba.

“Hili ni jambo la mfano kwa timu zingine, kuzingatia yale yanayoagizwa na  Serikali, ambapo hivi karibuni Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Damas Ndumbaro aliwaita Simba na kuwataka kufanyia kazi mambo kadhaa ya katika yao na inawapongeza na inawatakia kila la kheri,” alisema Mihayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: