Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba mtullie sasa, mfanyieni hili Benchikha..!

BENCHIKHA New.jpeg kocha Abdelhak Benchikha

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benchikha ni kocha mwenye CV kubwa anaonekana kafundisha timu kubwa zenye mafanikio makubwa Afrika na analifahamu vyema soka la Afrika lakini amekuja kipindi kibaya ambacho tayari timu ya Simba imevurugika haina muunganiko unaelekewa.

Kocha huyo amefika kipindi ambacho hata wakifanya usajili basi ni kwa asilimia ndogo maana ni dirisha dogo lililopo mbele yake hawezi kufumua kikosi kizima ama hawezi kupata wachezaji bora kwa sasa maana wengi wapo kwenye mikataba na timu zao.

Amekuja kipindi ambacho atahitaji utulivu na kuwatumia zaidi wachezaji waliopo na sio wale anaowahitaji yeye kwa wakati huo, waliopo ni kuhakikisha kwenda nao katika mbinu zitakazompa matokeo mazuri.

Wakati yote hayo anakumbana nayo Benchikha basi viongozi na mashabiki wa Simba wanahitaji kuwa na utulivu wa hali ya juu na kuvumilia kila hali, maana hata mashabiki wakipiga kelele za kumfukuza kama hawaoni matokeo mazuri hazitasaidia kutokana na nyakati zilizopo.

Benchikha na benchi lake wana kazi ya ziada ya kufanya ndani ya Simba ili kukitengeneza kikosi chake maana ukiachana na kiwango chao lakini inaonekana ndani ya timu hakuna ule umoja, hivyo ni kazi ya ziada kuurejesha umoja na kila mmoja kujiona ni sehemu ya timu.

Simba inahitaji mafanikio makubwa zaidi lakini kwa kinachoendelea sasa wanapaswa kuanza kusaka mafanikio makubwa msimu ujao ili msimu huu wampe nafasi kocha wa kujenga na kutatua yaliyopo kwa wachezaji wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: