Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba mechi 7, dakika 630 bila ushindi

Ngoma Simbaaaa Ms.jpeg Simba mechi 7, dakika 630 bila ushindi

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa, Simba wameandika rekodi yao kwenye anga hilo kwa kukomba dakika 630 sawa na mechi saba bila kuambulia ushindi.

Kwenye mechi hizo, mbili ilikuwa ni African Football League, (AFL) na tatu Ligi ya Mabingwa Afrika na mbili Ligi Kuu ya NBC. Katika mechi tano za Kimataifa, tatu wamecheza nyumbani na mbili ugenini.

Katika mechi za AFL, ilikuwa hivi; Simba 2-2 Al Ahly na Al Ahly 1-1 Simba. Simba iligotea hatua ya robo fainali kwa kanuni ya bao la ugenini.

Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, mechi ya kwanza ilikuwa Power Dynamos 2-2 Simba na Simba 1-1 Power Dynamos. Ni faida ya mabao ya ugenini yaliwapa fursa Simba kutinga hatua ya makundi.

Kwenye Ligi Kuu ya NBC, Simba waliambulia kichapo cha bao 5-1 kutoka kwa wapinzani wao Yanga, kisha sare ya bao 1-1 kutoka kwa Namungo.

Mchezo wa kwanza hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika ambao unakamilisha dakika 630, ilikuwa Simba 1-1 ASEC Mimosas.

Mechi tano mabao ya kufunga ni 9 na wamefungwa mabao 13. Hivyo Simba kufunga kimataifa ni kawaida yao na kufungwa pia ni kawaida yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: