Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kushusha straika wa Sh870 milioni

Mo Dewji: Tunahitaji Golikipa Mwingine Simba Rais wa Heshima wa Simba SC, Mohamed Dewji

Sat, 13 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Zikisalia siku mbili kufungwa dirisha la usajili, Simba mezani kwao wana majina matatu ya washambuliaji tofauti lakini mmoja kati ya hao ndio anawaumiza kichwa.

Mshambuliaji ambaye Simba wanamtaka anayetakiwa na kocha wao bajeti yake inawaumiza vichwa vigogo hao na sasa imekabidhiwa kwa tajiri wao Mohamed Dewji MO.

Taarifa kutoka vigogo wa juu wa Simba ni kwamba Benchikha amewakabidhi jina la mshambuliaji huyo ambaye hawakutaka kumtaja jina anayehitaji Dola 350,000 (Sh875 milioni) huku mshahara wake uwe Dola 20,000 (Sh50 milioni kwa mwezi).

Benchikha hakubaliani na viwango vya washambuliaji alionao ambapo kwa malengo aliyopewa na uongozi wake amesisitiza mashine hiyo ya mabao ishushwe kwenye kikosi chake.

Simba hadi sasa imesajili wachezaji watatu ambao ni wazawa Ladack Chasambi akitokea Mtibwa, Salehe Karabaka JKU na wa nje ni Babacar Sarr.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: