Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba inaua vipaji vya wazawa - Shabiki

Simba Hsgsgsh.jpeg Simba inaua vipaji vya wazawa - Shabiki

Mon, 28 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwasasa Simba sc ni kama wana kauli mbiu yao ya Njoo Tukupoteze tukuache Kuanzia msimu wa 2021/22 hadi leo hii hakuna Mzawa aliyesajiliwa na Simba sc kisha akaaminiwa kwenye kikosi.

Wengi wao wanasajiliwa wanasugua bench , wanaachwa , mwisho wa siku mchezaji akipata team nyingine anaenda kujitafuta kama ambavyo Mhilu leo hii anajitafuta kurejesha ule ubora wake wa 2020/21.

Wazawa wanao aminika Simba sc ni wale ambao walijijengea utawala wao mapema kipindi hiko , lakini suala kuu la Simba sc kuendeleza vipaji limekuwa adimu sana

Kwa upande wa Yanga hali ni tofauti, wachezaji wazawa wanapata nafasi ya kucheza, utamuona Mauya, Nkane, Job, Mwamnyeto, Kibwana, Kibabage, Metacha, Mzize na wengine wanapata nafasi lakini kwa Simba ni huzuni kubwa kwa wachezaji wazawa.

Kocha Nabi alikuwa anawapa nafasi wachezaji wote wa Yanga, Gamondi pia anawapa nafasi wachezaji wa Yanga, hakuna mchezaji wa Yanga anasugua benchi kwa muda mrefu labda awe na majeraha.

Kwa upande wa Simba, Kenedy Juma kucheza ni mpaka Inonga aumie, Ally Salim mpaka Manula aumie, kwa nini wachezaji wazawa wa Simba walio wengi wao wanaonekana takataka? Mbona kipindi Cha mgunda walikuwa wanapata nafasi?

Duchu, Mwenda, Kenedy, Kazi, Mohammed Musa, Chilunda, Hussein Abel, Jimmyson Mwanuke, hawa kupata nafasi ni mpaka Mchezaji tegemezi aumie.

Si kwamba hawa wachezaji hawana uwezo kabisa wa kuanza hata mechi dhidi ya Coastal Union, na kama hamuwaamini mlikuwa mnawasajili wa nini? Na nini maana ya kikosi kipana?

Ikitokea hawa wachezaji wameanza kushuka viwango viongozi na Kocha watambue wanhusika kwa kiasi kikubwa sana kuwapoteza hawa wachezaji.

Walimchukua Mhilu wakaja kumpoteza, wakamchukua Mwenda hawampi nafasi, wamemchukua Musa kutoka Zanzibar hawataki kumpa nafasi, Simba ndiyo timu yao wasipopata nafasi hapo watapata nafasi timu gani?

Hivi umejiuliza kwa nini Msimu uliopita Yanga iliongoza kuwa na wachezaji National Team? Ni kwa sababu wachezaji wengi walikuwa wanapewa nafasi, unapompa mchezaji nafasi kunatengeneza ajiamini, unapojiamini huzaa perfomance nzuri.

Denis Nkane leo kapata nafasi anapambania timu, hii inampa moyo tena akipata nafasi atafanya vizuri zaidi. Majuzi kati Simba sc ilishinda gosi nne, lakini bado wachezaji kama kina Duchu, Mwenda hawapewi nafasi wakati kimahesabu ni mechi ambayo wangeweza kucheza na kufanya jambo.

Mdathir Yahya kama si kupewa nafasi leo hii sidhani kama angelikuwa na kiwango hiki, lakini hapo hapo msimu ujao mtawaacha na kuwatoa kwa mkopo ni ilihali tayari mshaua vipaji vyao kwa nini?

Ninaamini sana uwezo wa bwana mdogo kutoka Zanzibar lakini unakuta Bocco anapata nafasi dogo hapati jkwa nini? Viongozi wa Simba, mashabiki wa Simba mfikishieni taarifa kocha Robertinho kwamba hawa wachezaji wanapaswa kuaminiwa na kupewa nafasi Simba ndiyo timu yao?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: