Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba inahitaji utulivu mkubwa kwa sasa

Mo Dewji: Tunahitaji Golikipa Mwingine Simba Simba inahitaji utulivu mkubwa kwa sasa

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naweza kusema hali sio shwari sana ndani ya klabu ya Simba na siyo tu baada ya kichapo walichopata kutoka kwa watani zao, Yanga waliowafungwa mabao 5-1 wikiendi iliyopita. Hali ndani ya Simba si nzuri kwa muda mrefu ila ni kwa vile tu timu inapata matokeo mazuri kwenye mechi nyingi wanazocheza, hakuna kelele nyingi huku mitaani.

Simba inapata matokeo mazuri uwanjani ingawa mashabiki hawaridhiki na kiwango inachoonyesha lakini wanapozwa tu na mafanikio. Lakini kinachosemwa ni kwamba Simba kuna matatizo makubwa ya kiuongozi ambayo ni anguko kwa timu ambalo hasa ndilo tunaliona.

Kinachowauma na kuanza kuonekana zaidi kwamba mambo si shwari kwa mabosi wa klabu ni hiki kipigo, vinginevyo mambo yangeendelea kwenda kimyakimya. Sasa ni kama kila kitu kipo wazi, tetesi ambazo zinaweza kuwa kweli ama uongo zinazungumzwa, hivyo maswali ni mengi kwa mashabiki lakini ndani ya viongozi hao hao nao hawajatulia kwani wanahaha kuona kwamba mambo yanatulia.

Mabosi wa Simba hawaishi kufanya vikao kuona ni namna gani upepo utatulia ili hata dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa wawe na utulivu wa akili kuongeza wachezaji wenye msaada kwao. Simba si kwamba haijasajili, imesajili lakini usajili wao hauna faida yeyote zaidi ni wachezaji wawili hasa wa kigeni ndiyo wameonyesha ubora wao Fabrice Ngoma na Che Malone, wengine bado mwendo ni mdogo mdogo tofauti na wengi waliotarajia.

Kikosi cha Simba ukikiangalia nguvu wanayoitumia sasa ni ile ya msimu uliopita kwa wachezaji ambao ni wale wale wanaoipambania timu miaka yote, jambo ambalo wengi wanajiuliza kwanini viongozi wa Simba wanashindwa kufanya maamuzi ya kusajili wachezaji mbadala.

Timu imejaa mafaza ambao wana uamuzi na nguvu ya kuamuru nini wanataka. Kwa Simba hii ambayo imeondoka kwenye mfumo wa kizamani haipaswi kukumbatia hayo. Inatakiwa kuwa na wachezaji wanaojua na kutambua majukumu na sio kuleta urafiki.

Simba ijitathimini kwani ina jukumu kubwa mbele, ligi inaendelea na inakwenda kucheza mechi ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kujivuruga kwao na kukosa utulivu kunaweza kuwaharibia huko mbele…

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: