Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba imechelewa sana kwa Ngoma

Fabrice Ngoma Mapinduzi.jpeg Kiungo wa Simba SC, Fabrice Ngoma

Fri, 12 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mashabiki wa Simba hivi sasa wanachizika na kiwango bora cha kiungo Fabrice Ngoma ambaye timu hiyo ilimsajili kabla ya kuanza kwa msimu huu akitokea Al Hilal ya Sudan.

Ngoma ni mtaalam eneo la kiungo hasa uwezo wake wa kuchezesha timu kwa kupiga pasi ndefu na fupi ambazo zimekuwa zikiwafikia walengwa kwa usahihi.

Na hiyo ndio sifa mojawapo ya mchezaji anayecheza nafasi ya kiungo kwamba lazima awe na uwezo wa kupiga pasi zinazofika. Kama huwezi kufanya hivyo sio mbaya ukaacha kucheza kama kiungo na kukimbilia nafasi nyingine au kama vipi achana kabisa na soka.

Hicho kiwango chake ndio kimemfanya awe tegemeo chini ya makocha wawili tofauti ambao wamefundisha Simba msimu huu, akiwa na Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ambaye baada ya kutimuliwa kwake akamuachia Abdelhak Benchikha.

Msimu uliopita, viungo Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin walikuwa wamejihakikishia nafasi kikosi cha Simba lakini uwepo wa Ngoma msimu huu umewafanya wawili hao wacheze kwa kupishana.

Ngoma anayafanya hayo akiwa ndio anatimiza umri wa miaka 30 ambayo kisoka tunaanza kumhesabu kuwa ameanza kuzeeka kwani umri ambao mchezaji anapaswa kuwa wa moto zaidi ni ule wa kuanzia miaka angalau 20 hadi 27.

Maana yake Simba inamfaidi Fabrice Ngoma katika kipindi ambacho ameshaanza kuwa maji ya jioni na kipindi sahihi alichohitajika na kingeifanya timu hiyo inufaike zaidi na kiwango na ubora wa kiungo huyo, haikuweza kumpata kwa vile alikuwa anazitumikia timu ambazo zilimpa malisho ya kijani zaidi.

Na huwezi kuilaumu wala kuinyooshea kidole Simba kwani jambo lililo wazi kwamba timu zetu bado hazijawa na misuli mikubwa ya kiuchumi kuweza kushindana katika soko la usajili wa wachezaji mahiri na walio katika umri sahihi pindi wenye fedha nyingi wanapojitokeza kumuwania mchezaji husika.

Kama huyu Ngoma ndio anacheza hivi sasa akiwa anamaliza soka lake, Simba ingempata akiwa wa moto ingenufaika sana.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: