Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba hatuna wachezaji wenye pumzi - Mchome Mapovu

Kapombe Na Tshabalala Mohamed Hussein Simba hatuna wachezaji wenye pumzi - Mchome Mapovu

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki kindakindaki wa Simba SC, Mchome Mapovu amesema kuwa wachezaji wa timu hiyo hawana pumzi ya kutosha kupanda na kushuka, jambo ambalo linawafanya wafungwe mabao mengi ya counter attack.

Mchome amesema hayo baada ya Simba kukubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Tanzania Prisons juzi katika uwanja wa CCM Jamhuri mjini Morogoro.

“Mfumo anaochezesha ni mgumu, anataka beki namba 2 na 3 wapande wakashambulie, zikipigwa counter attck nani anakuja kuziba? Simba hatuna wachezaji wenye pumzi hiyo kupanda na kushuka.

“Yanga wana wachezaji wenye uwezo huo, Yao Kouassi na Kibabage wana uwezo wa kupanda na kushuka kwa wakati, sisi tunalazimisha lakini hatuna wachezaji hao, mwalimu muda wote ana hasira anarusha tu mikono wakati yeye ndiye anapanga kikosi.

“Mabao yote tunayofungwa Simba yanatokea pembeni mwa uwanja, wachezaji wakipokonywa mpira wakati wa kushambulia, wanatembea, kwa nini msifungwe?,” amesema Mchome.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: