Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga uzalendo kwanza CAF

Simba, Yanga Warejea Ligi Kuu Jumamosi Simba, Yanga uzalendo kwanza CAF

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kauli ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro, kuwapiga marufuku mashabiki wa Simba na Yanga, kuacha tabia za kusapoti wageni wakati wa mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika, imeungwa mkono na wanamichezo.

Ndumbaro aliyasema hayo jana usiku, wakati akichangia mjadala wa Mwananchi Space, ulioandaliwa na Mwananchi Communications Ltd, wenye mada isemayo 'Ipi nafasi ya Simba, Yanga kwenye vita ya kusaka nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga inakutana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Simba na Al Ahly ya Misri kusaka tiketi ya kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Hatutawaachia Yanga, Simba wala Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kushughulika na mashabiki wanaowasapoti wageni, hili ni jambo la kitaifa, linahitaji uzalendo zaidi, sitarajii kuona wakivaa jezi za upinzani uwanjani," alisema na kuongeza;

"Ikiwezekana Jumanne ijayo, tutakaa na TFF, Simba na Yanga, ili kujua wanajipangaje kwa ajili ya mechi zao, Tanzania imeandika rekodi ni nchi pekee kwa mwaka huu kuingiza timu mbili, pia mara ya kwanza timu hizo kutinga robo fainali ya CAF kwa pamoja, hiyo ni hatua kubwa."

Jambo lililoungwa mkono na staa wa zamani wa Yanga na Stars, Edibily Lunyamila aliyesema serikali tangu mwanzo ipo bega kwa bega na klabu hizo, hivyo mashabiki ni suala la kuelewa, akisisitiza utani sio uadui.

"Nakumbuka mwaka 1993, Simba ilifika fainali ilicheza dhidi ya Stella Abidjan ya Ivory Coast, mashabiki wote walikuwa wanashangilia Simba, wakiwa na vibendera vidogo vya taifa, baada ya kufungwa mabao 2-0 mashabiki wa Yanga wakageuka na kuanza kuwashangilia wageni," alisema na kuongeza;

"Uzalendo unawezekana, hakuna mtu anayeweza kumpangia mtu mapenzi, ila kuna ulazimika gani, kama Simba inacheza na Al Ahly Yanga kuwashangilia wageni, ama Yanga inapocheza na Mamelodi Sundowns wafuasi wa Simba kushangilia wapinzani, hilo ni jambo la kitaifa lipewa nguvu."

Kwa upande wa staa wa zamani wa Simba, Zamoyoni Mogella alisema "Uzalendo ni jambo muhimu, natamani kuona timu hizo kutinga nusu fainali, mashabiki wakiwasapraizi wageni kwa kuungana, hilo litasaidia kuondoa kujiamini kwa wageni."

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha nchini (RT), Suleiman Nyambui alisema "Ni ushabiki ushamba kujipendekeza kwa wageni, naamini mitazamo ya mashabiki ikibadilika, kuna uwezekano Simba na Yanga zikaanza kunyakua mataji ya Afrika na itakuwa nchi inayoogopwa."

Kocha wa Dodoma Jiji, Francis Baraza alisema; "Kauli ya Waziri Ndumbaro, ikizingatia na makocha wakajipanga, wachezaji wakajituma, Tanzania itakwenda kuandika historia nyingine, kwenye mashindano ya CAF."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: