Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Tumeshajua tunapokosea

Ntibanzonkiza Kinara Wa Mabao Simba SC Simba: Tumeshajua tunapokosea

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema ni makosa yao wenyewe ndiyo yanawafanya washindwe kuibuka na ushindi kwenye michezo yao ya hivi karibuni.

Simba ambayo haijapata ushindi katika mechi minne mfululizo kwa sasa imefikisha pointi 46 katika michezo 20, huku ikiwa nafasi ya tatu, huku mchezo ujao ni dhidi ya watani wao wa jadi Yanga ambao utachezwa Aprili 20,2024 katika uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya kumi na moja jioni.

“Wachezaji wakiacha makosa madogo madogo wanayoyafanya, uwezekano wa kupata ushindi kwenye mchezo huo ni mkubwa mno. Tuwaamini wachezaji wetu, tuwape moyo wakatupiganie.

“Tukipoteza mchezo huo aibu inabaki kwetu sisi, hawa wachezaji wote wataondoka Simba, sisi tutabaki hapa hapa na fedheha tutabaki nayo wenyewe kwamba tulifungwa mara mbili ndani ya msimu mmoja.

“Twende tukapambane kuhakikisha Aprili 20 tunapata ushindi. Ninaamini timu ya kupata ushindi tunayo na uwezo tunao, kila kitu tunacho lakini tunahitaji nguvu ya Wanasimba.

“Hata ukiwa na makasiriko ya kujaza dunia nzima, tukipigwa Jumamosi utakasirika zaidi, bora tukaungana wote kwenda kuipigania Simba yetu," amesema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: