Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Tumejiandaa kushinda ugenini

Matola Kusoma Kocha Msaidizi wa Simba SC Seleman Matola

Tue, 20 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema wanakwenda Ivory Coast kwa jambo moja tu, kuhakikisha wanaipata ushindi dhidi ya Asec Mimosas.

Simba imeondoka leo alifajiri kuelekeza Ivory Coast kwa ajili ya mchezo muhimu wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi utakaopigwa Ijumaa ijayo.

Akizungumza na Mwananchi, Matola alisema wamejiandaa kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo huu kwa kuwa hakuna jambo lingine linaweza kuwasaidia kuvuka kwenda robo fainali.

Alisema anafahamu wapinzani wao wameshafuzu, lakini siyo kigezo kuwa wanaweza kupanga kikosi dhaifu kwenye mchezo huu kwa kuwa wanataka kuweka rekodi.

"Tunakwenda na tahadhari zote tukifahamu kuwa jambo pekee ambalo linaweza kutupa mwanga wa kufuzu hatua ya robo fainali ni kuhakikisha tunapata ushindi kwenye mchezo huu.

"Asec tayari imeshafuzu kwa kufikisha pointi 10, lakini hili siyo jambo ambalo linatakiwa kutufanya tuamini mchezo utakuwa mwepesi, hii ni timu kubwa yenye heshima kwenye soka la Afrika, lazima tuamini kuwa tunatakiwa kupambana mpaka mwisho.

"Kwenye soka siku zote timu inapata ushindi kama imefanya maandalizi ya kutosha, sisi tumejiandaa kwa ajili ya mchezo huu na hatuna shaka," alisema Matola kocha wa zamani wa Lipuli ya Iringa.

Asec inaongoza Kundi B ikiwa na pointi 10, Simba inashika nafasi ya pili ikiwa nazo tano, inafuatiwa na Jwaneng Galaxy na Wydad Casablanca tatu zote zikiwa zimebakiza michezo miwili.

Mbali na mechi hiyo ya Simba, Ijumaa Al-Hilal iliyopo mkiani mwa Kundi C itacheza na vinara Petro de Luanda, wakati Medeama itavaana na Al Ahly SC zote za kundi D.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: