Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Singida Fountain waoneshana ubabe usajili wa beki huyu

IMG 4461 Che Fondoh Malone.jpeg Che Fondoh Malone Jr

Mon, 26 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tetesi katika kipindi hiki cha usajili zinasema Klabu ya CottonSports FC ya Cameroon imeripotiwa kuitaarifu Simba SC ya Tanzania kuwa beki Che Fondoh Malone Jr atauzwa ikiwa dau la dola laki moja na nusu (Tsh milioni 357) litatua mezani.

Che Malone (24) raia wa Cameroon tayari imefikia makubaliano ya maslahi binafsi kwa ajili ya kusaini mkataba wa kuwatumikia Wekundu hao wa Msimbazi msimu ujao.

Hata hivyo Klabu ya Singida Fontaine Gate nayo iliripotiwa kuweka ofa mezani katika juhudi za kuwazidi ujanja Simba SC na kumsajili beki huyo ambaye mkataba wake na CottonSports utafikia ukomo wiki chache zijazo ingawa Cotonsport haitaki kumwachilia.

Simba inasaka kwa nguvu zote mlinzi wa kati baada ya kuachana na beki wake Mohammed Outtara ambae alishindwa kuonesha kiwango klabuni hapo.

Je msomaji unamuona Malone Msimbazi au kwa Walima Alizeti?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: