Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba SC, nyakati za neema zilivyogeuka mashaka

Simba Simba SS Simba SC, nyakati za neema zilizvyogeuka mashaka

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kile kibubu kilichokuwa kinabeba neema kimejaa mashaka. Mnyama simba ni kama anatembea kwenye tanuli la moto, huku mpinzani wake akidundika kwa maringo.

Nyakati za neema zimegeuka kuwa nyakati za mashaka msimbazi, vifua vya mashabiki vilivyojaa matumaini vimeanza kuchoka kuisubiri kesho bora.

Bila shaka nyakati za mashaka zimetanda msimbazi. Wakati giza linazidi kufunika matumaini ni dhahiri ni muda wa kukubaliana na uhalisia umefika

Mwaka 2006 Don Florentino Perez na ubishi wake wote lakini aliamua kushusha mikono chini na kuondoka zake pale Real Madrid sababu kubwa ni "project' yake kushindwa kufanya vizuri.

Ulikuwa ni msimu wa tatu bila taji lolote lile kwa Real Madrid, Florentino Perez alikuwa na wakati mgumu, baada ya kupoteza na timu iliyekuwa inaburuza mkia Real Mallorca aliamua kuitisha board ya Real Madrid na kujiuzulu zilikuwa nyakati za mashaka Real Madrid.

Baada ya miaka kadhaa kupita Florentino Perezi alirudi na nguvu mpya na project mpya ndio hii inayotesa kwa sasa barani ulaya.

Nyakati kama hizi ziliwahi kuisogelea klabu ya Yanga, ulikuwa wakati ambao kila tamu iligeuka chungu, huku msimbazi ulikuwa ni wakati wa neema, ni GSM na mipango yake mizuri ndio iliirejesha Yanga kwenye kilele cha ubora wao.

Ni wakati wa Simba kuunda 'project' mpya umewadia, ile project ya kuunda project mpya kwa kutumia vijana iliishia kwenye viganja vyao wenyewe Pape Sakho, Peter Banda, wote waliondoka zao.

Nilitamani project mpya iishi kwenye mawazo ya Benchikah bahati mbaya alikuwa kocha sahihi kwenye muda usio sahihi, Ameondoka.

Kuunda project mpya ni pamoja na kuwabakiza wachezaji wako bora. Tp Mazembe walifanya hivyo, ni muda Simba kuwalinda wachezaji bora wasiondoke ili project mpya iishi ndani yao.

Mnyama atanyanyuka kutoka kwenye maumivu, sio mbali ni karibu zaidi unavyofikilia. Nguvu moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: