Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba SC kwenye Dunia yao ya maamuzi ya kustaajabisha

Bqleke Phirii00 Simba SC kwenye Dunia yao ya maamuzi ya kustaajabisha

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati duniani ikistaajabu ubora wa Meddie Kagere, Ni Simba ndio waliamua kukatisha simulizi tamu ya ndoa kati ya Meddie Kagere na kuzitendea ukatili nyavu.

Aliwafurahisha wana msimbazi haswa. Misimu miwili goli 20+ ligi kuu ni binadamu wachache sana wanaweza kufanya hivyo.

Ilinishtusha ile taarifa ya Meddie Kagere kuachwa. Hata mwendawazimu kwenye kilele cha uwendawazimu wake huenda asingeweza kuliakifu jambo lile.

Kocha mpya alivyowasili alimuacha Meddie Kagere. Alimuacha kwa hoja dhaifu. Ety hakuweza kumiliki mpira

Mbaya zaidi mbadala wake "Chris Mugalu" alimiliki mpira lakini hakuweza kufikia hata robo ya ubora wa Meddie Kagere kwenye kucheka na nyavu

Binafsi nilimkumbuka Meddie Kagere kila Chris Mugalu alipolikaribia goli.

Hili lilikuwa tukio la pili kuniumiza, tukio la kwanza ni lile la kumuacha Hamis Tambwe akiwa ametoka kuwa mfungaji bora. Ni uwendawazimu!

Viongozi wa simba hawajaacha kunistaajabu, Wametudanganya tena kwa Jean Baleke na Moses Phiri.

Kuna ukatili unafanyika na viongozi wa simba ili kumchinja mbuzi wa kafala.

Huenda hiki kinachomtafuna chama ni chuki binafsi za baadhi ya watu. Njia chafu kama hizi wamewahi kupitia " Meddie Kagere", " Beno Kakolanya", "Moses Phiri", " Hamis Tambwe".

Ni kamali nyingine Wameisukuma viongozi wa simba katikati ya msimu wanawaacha washambuliaji wake bora wa misimu miwili iliyopita. Mbaya zaidi hatujajua wachezaji waliosajiliwa kama wataliweza vyema soka la Tanzania.

Jean Baleke, Moses phiri wanaondoka. je Pa omar jobe na Kouablen wataweza kuziba nafasi tusubiri muda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: