Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba SC: Tuna hamu na Coastal Union, wasitupangie kipa!

Ally Salim X Lakred Tuna hamu na Coastal Union

Tue, 19 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha timu ya Simba kimerejea nchini jana Jumatatu, Septemba 18, 2023 wakitokea nchini zambia ambako walikwenda kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Power Dynamos ambapo walitoa sare ya bao 2-2.

Akizungumza leo, Meneja wa Habari na mawasiliano wa Kalbu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kikosi hicho kimeelekea kambini moja kwa moja kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Coastal Union utakaopigwa keshokutwa Alhamisi, Septemba 21, jijini Dar es Salaam.

“Coastal Union tunawakaribisha, tulikuwa na hamu nao kweli tangu tulivyoomba tucheze mechi na wao kama wiki mbili zimepita, mambo yakawa mengi, mara wamevunja kambi.

“Kifupi ni kwamba walikula nyoya, lakini sisi ni people, tumekutana, Alhamisi tutakutana nao kwa ajili ya kwenda kuwapelekea moto Wagosi wa Kaya.

“Kuhusu kipa Ayoub Lakred, Coastal wasitupangie, anaweza akadaka kipa yeyote yule ambaye Simba SC tutamuamini,” amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: