Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba SC, Singida FG hatumwi mtoto dukani

Simba Vs Singida Chama.jpeg Simba SC, Singida FG hatumwi mtoto dukani

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ligi Kuu itaendelea tena kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi wakati Simba ikiikaribisha Singida Fountain Gate huku kila kocha akitamba kuibuka na ushindi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kocha msaidizi wa Simba, Selemani Matola alisema hadi sasa morali ya wachezaji iko juu na wanaamini kama benchi la ufundi wamerekebisha baadhi ya makosa.

"Siku zote hakuna mechi rahisi kati ya Simba na Singida inatupa ugumu sana, tumejipanga pamoja na ubora wao ili kushinda, tutachukua tahadhari na tutahakikisha hatufanyi makosa," alisema Matola.

Kocha wa Singida FG, Ngawina Ngawina alisema Simba ni timu nzuri lakini dakika 90 za Uwanja wa Chamazi zitaamua mshindi.

"Tupo tayari kwa mchezo na tunawajua vizuri Simba ni timu kubwa, tumeona udhaifu wao na ubora wao, tumepata pointi moja kwenye michezo minne, tumekaa mazoezini ya kurekebisha makosa yetu, tutaingia kwenye mechi kwa tahadhari kubwa," alisema Ngawina.

Kipa wa Singida, Beno Kakolanya alisema kuwafahamu wachezaji wa Simba sio kigezo cha wao kupata matokeo na wataingia kwa tahadhari ili kutoruhusu bao.

"Mpira umebadilika sio kwamba kuwafahamu baadhi ya wachezaji wa Simba ndio itakuwa sababu, ninachofahamu wachezaji wenzangu wana morali ya mechi na naamini tutafanya vizuri," alisema Kakolanya, aliyejiunga na Singida FG akitokea Simba.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: