Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Njooni tunaanza upya

Mataa Kikosini Simba: Njooni tunaanza upya

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baadhi ya mashabiki wa Simba wamesikika wakitamba kuwa baada ya kipigo kutoka kwa watani zao, Yanga, Jumapili iliyopita chama lao linarejea kufanya mambo mazuri

Ligi Kuu Bara inaendelea tena leo kwa mchezo mmoja kupigwa kwenye Uwanja wa Uhuru ambapo Simba iliyochapwa mabao 5-1 na Yanga itakuwa ikiikaribisha Namungo.

Wakati Simba ikiingia mchezoni kutaka kupata matokeo chanya yatakayorejesha furaha kwa mashabiki wake, upande wa Namungo ilitoka suluhu mechi ya mwisho na Coastal Union Novemba 1, kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Simba inaingia mchezoni pia ikiongozwa na Kaimu Kocha Mkuu, Dani Cadena na msaidizi Seleman Matola baada ya Kocha Mkuu Roberto Oliveira ‘Robertinho’ kutimuliwa juzi kufutia kichapo.

Robertinho aliyejiunga na Simba Januari 3, mwaka huu akitokea Vipers ya Uganda alidumu siku 308 huku akiondoshwa pia na kocha wa viungo Mnyarwanda Corneille Hategekimana.

REKODI ZAIBEBA

Tangu Namungo ipande Ligi Kuu 2019/2020, huu ni mchezo wa tisa kukutana na Simba ambapo kati ya minane iliyocheza haijawahi kushinda kwani imepoteza mitano na sare mitatu huku ikifungwa mabao 15 na kufunga sita.

Katika michezo hiyo ni mmoja tu ambao haujatoa bao ambao ni ule ziliotoka suluhu Julai 8, 2020 huku mechi ya mwisho iliyopigwa Uwanja wa Mkapa Simba ilishinda 1-0, lililofungwa na straika Moses Phiri.

Namungo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Denis Kitambi itakuwa na kibarua cha kuvunja unyonge uliotawala ingawa amekuwa na rekodi nzuri ya kutopoteza mchezo kwani kati ya miwili aliyoiongoza ameshinda mmoja na kutoka sare mmoja.

MAK0CHA

Akizungumzia mchezo huo, Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Dani Cadena alisema: “Tunahitaji kurejesha morali na imani ya mashabiki zetu, siwezi kusema kutakuwa na mabadiliko makubwa isipokuwa tutaangalia tu na utimamu wa kila mchezaji.”

Kwa upande wake Kitambi alisema wanatambua ubora wa wachezaji wa Simba, lakini lengo lao ni kuondoka na pointi tatu

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: