Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Ngoja tuwaonyeshe

Simba Players Chama Simba: Ngoja tuwaonyeshe

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku nne za mtego kwa Simba kwenye Ligi Kuu Bara zinaanzia leo katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya wakati itakapokabiliana na Tanzania Prisons kuanzia saa 10:00 jioni, huku kocha wa timu hiyo, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amewaambia mashabiki kuwa ngoja tuwaonyeshe.

Simba itavaana na Prisons katika mechi ya kwanza ya msimu huu ikiwa ni ya kwanza kwa kocha Robertinho dhidi ya maafande hao, huku akiwa na presha kubwa kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo kama ilivyo kwa Minziro ambaye hajaonja ushindi kwenye mechi za ligi kwa msimu huu hadi sasa.

Presha ya nje ya uwanja inayoikabili Simba licha ya kutopoteza mechi yoyote msimu huu, inailazimisha kupata ushindi leo na kisha mchezo utakaofuata keshokutwa Jumapili, ili kuliweka salama benchi lake la ufundi chini ya Robertinho, lakini ili kutoathiri mbio zao za kuwania ubingwa wa ligi hiyo msimu huu.

Ukiondoa presha hiyo hasa kutoka kwa baadhi ya mashabiki ambao wanalalama kuwa Simba haichezi vizuri, ndani ya uwanja imeendelea kupata matokeo mazuri hasa katika Ligi Kuu ambapo imeshinda mechi zote tatu ilizocheza dhidi ya Mtibwa Sugar, Dodoma Jiji na Coastal Union, ikifunga mabao tisa na kuruhusu mawili tu kutinga nyavuni mwa lango la timu hiyo.

Bila ya shaka ni mechi ambayo haitokuwa rahisi kwao na inategemewa kuwa na ushindani mkali kutokana na wapinzani wao kutokuwa na mwenendo mzuri katika mechi tatu za mwanzo dhidi ya Singida Big Stars, Azam FC na Tabora United ambazo imetoka sare moja na kupoteza mbili, huku ikifunga mabao mawili tu na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara sita.

Simba inaingia katika mechi ya leo ikiendelea kuwakosa Aubin Kramo, Aishi Manula aliyeanza kurejea mazoezini baada ya kupona majeraha ya muda mrefu ya nyama za paja na mwingine ni beki Enock Inonga anayeuguza jeraha la ugokoni, lakini ina nguvu mpya ya urejeo wa Luis Miquissone aliyekosa mechi iliyopita dhidi ya Power Dynamos.

Kiujumla Simba imekuwa na historia nzuri dhidi ya Prisons kwani imepata ushindi mara nyingi zaidi katrika mechi baina yao na uthibitisho wa hilo ni michezo 10 iliyopita ya Ligi Kuu ilizozikutanisha, kwa Mnyama kuibuka wababe mara tano ikifunga mabao 12, Prisons ikipata ushindi mara mbili na kufunga mabao manne huku timu hizo zikitoka sare mara tatu.

Ushindi kwa Simba leo utaifanya ifikishe idadi ya mechi 27 mfululizo ilizocheza bila kupoteza, lakini itapanda hadi kileleni na kuongoza msimamo kwani itafikisha pointi 12 na kuing;oa Azam yenye pointi 10.

Akizungumza pambano hilo, Robertinho alisema licha ya mashabiki kulalamika, lakini kikosi hicho kina uwezo wa kupata matokeo kwenye uwanjan wowote na hilo litathibitishwa leo kwenye Uwanja wa Sokoine.

Kocha huyo alisema timu hiyo inacheza kwa mbinu kutokana na aina ya mchezo wanaokutana nao akisema kuwa waootilia shaka kiwango kwenye mchezo uliopita wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos wao walihitaji kufuzu makundi jambo ambalo walifanikiwa.

Kauli ya kocha huyo raia wa Brazil inakuja wakati baadhi ya mashabiki wakieleza kutofurahishwa na kiwango cha timu hiyo ambayo licha ya kufuzu hatua ya makundi ikibebwa na kanuni kwa matokeo ya jumla ya mabao 3-3 huku Simba ikinufaika kwa wastani wa mabao mawili ya ugenini.

Wekundu hao katika mechi ya kwanza dhidi ya Dynamos waliyocheza ugenini walimaliza kwa sare ya 2-2 huku mchezo wa marudio katika Uwanja wa Azam Complexm, Chamazi Dar es Salaam ukiisha kwa 1-1 na kuwaondoa wapinzani hao kutoka nchini Zambia.

Alisema anafahamu mechi dhidi ya Prisons itakuwa ngumu, lakini kwa maandalizi waliyofanya watashinda akibainisha kuwa kesho mashabiki watafurahi kwa soka litakalopigwa.

“Naamini watafurahi kesho (leo) kutokana na maandalizi tuliyofanya, tunafahamu mechi itakuwa ngumu dhidi ya wapinzani lakini tumejipanga, mechi iliyopita ilikuwa ya mbinu kufuzu makundi klabu bingwa na tulifanikiwa,” alisema kocha huyo Mbrazil, huku Kocha wa Prisons, Felix Minziro alisema: “Simba haina ugeni hapa kutokana na mashabiki wake kuwa kila kona, kimsingi tumejiandaa vyema na vijana wanapaswa kuzingatia nidhamu.” Minziro anasaka ushindi wa kwanza kwenye ligi msimu huu, lakini kulipa kisasi kwa Simba ambayo msimu uliopita ilishinda mechi zote, ikianza na ushindi wa 1-0 ugenini jijini Mbeya kisha kushinda nyumbani mabao 7-1.

Mechi zote hizo ilizoshinda Simba ilikuwa chini ya kocha Juma Mgunda ambaye alipokewa mikoba na Mbrazili Robertinho ambaye mchezo huo ni wa kwanza dhidi ya Prisons tangu ajiunge na timu hiyo mapema Januari mwaka jana na kuiongoza Simba kucheza mechi 14 mfululizo za ligi bila kupoteza, zikiwamo tatu za msimu huu.

Pia kipa wa Simba aliyewahi kuzidakia KMKM, Prisons na KMC, Hussein Abel alisema baada ya kukosekana uwanjani matarajio yake ni kuibukia leo Prisons akiahidi kuwa soka walilolikosa mashabiki linarejea upya, huku akisema ana matumaini na kuvuna pointi tatu.

Nahodha msaidizi wa Prisons, Benjamin Asukile alisema leo hawatarajii kurudia makosa tena akieleza kuwa wanachohitaji ni kubaki na ushindi baada ya kuusotea dakika 270 bila mafanikio.

Leo pia kwenye Uwanja wa Manungu Complex, Morogoro, Mtibwa Sugar itaialika Singida Big Stars.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: