Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Kila aliye mbele yetu ni halali yetu

Joash Onyango Beki Onyango akijifua

Fri, 2 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mechi mbili zimebaki kwa Simba kukamilisha ndani ya msimu wa 2022/23 ikiwa ni dakika 180.

Simba ipo nafasi ya pili kwenye msimamo na vinara wa ligi ni Yanga ambao wametwaa ubingwa wa ligi msimu huu.

Ikumbukwe kwamba Yanga inaiwakilisha Tanzania kwenye anga za kimataifa ikiwa ipo hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika na itapambana na USM Alger Juni 3. Kikosi hicho chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira kimeanza maandalizi kwa mechi hizo.

Ni dhidi ya Polisi Tanzania unaotarajiwa kuchezwa Juni 6 na ile kete ya pili na ya mwisho inatarajiwa kuchezwa Juni 9.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari ndani ya Simba amesema wapo tayari kwa mechi hizo mbili.

“Tunahitaji kufanya vizuri kwenye mechi zetu ambazo zimebaki na tunajua kutakuwa na ushindani mkubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi,”.

Miongoni mwa nyota ambao wameanza mazoezi ni pamoja na Onyango Joash, Henock Inonga, John Bocco, Jean Baleke.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: