Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Day, Jezi zinazinduliwa lini? Ahmed Ally ajibu!

Ahmed Ally Kis Simba Day, Jezi zinazinduliwa lini? Ahmed Ally ajibu!

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wakLabu ya Simba, Ahemd Ally amesema kuwa Jumamosi hii, Julai 15 watatangaza rasmi ni lini uzinduzi wa jezi mpya za timu yao utafanyika na lini Tamasha la Simba day litafanyika.

Ahmed amesema hayo kufuatia maswali kuwa mengi kuhusu matukio hayo huku mashabiki wakitaka jezi mapema kwani wapinzani wao Yanga tayari wameshatangaza na wameshaanza kuuza kwenye maduka.

“Maswali yamekuwa mengi kuhusu Simba Day kila mmoja anataka ajue ili apange ratiba yake, lakini maswali ambayo yanatukausha mate ni kuhusu lini tutazindua jezi. Sasa Jumamosi saa 5:00 asubuhi tutatoa matangazo yote kuhusu uzinduzi wa jezi na tarehe ya Simba Day.

“Niwahakikishie tu kwamba uzinduzi wa jezi utakuwa wa aina yake, haijawahi kufanyika duniani, hata tusipofanya sisi Simba watu wakaishi miaka elfu 10 mingine hakuna mtu atapata wazo la kufanya ambacho Simba tumepanga kufanya,” amesema Ahmed Ally.

Kikosi cha Simba chini ya Kocha Robertinho kiliondoka nchini Tanzania jana kuelekea Uturuki kwa ajili ya kambi maalum ya maandalizi kuelekea msimu mpya wa soka 2023/24.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: