Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Coastal Union tuna waheshimu ila tunataka alama tatu

Simba Rekodi CAF.jpeg Simba: Coastal Union tuna waheshimu ila tunataka alama tatu

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kikosi chao kimekwenda Tanga kwa ajili ya kusaka ushindi tu dhidi ya Coastal Union wala si kitu kingine.

Ahmed amesema hayo mara baada ya kutua Tanga kwa ajili ya mchezo wao utakaopigwa kesho Jumamosi katika Dimba la Mkwakwani huku Mnyama akiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons kwa kipigo cha bao 2-1.

“Tumekuja Tanga kwa kazi moja tu ya kupigania alama tatu dhidi ya Coastal Union. Mechi yetu itakuwa ngumu sana, Coastal wana timu bora na imara sana.

“Bahati mbaya ni kwamba Mnyama ametoka kujeruhiwa kwa hiyo hatuko tayari kupoteza mchezo huo wala kutoa sare, tutaingia kwa nguvu kubwa, tahadhari na heshima kubwa ili tupate matokeo chanya.

“Ukifungwa, ukipata matokeo mabaya lazima ujitathimi, tumefanya hivyo na kugundua wapi tulikosea. Hatuna muda wa kuanza kujilalamisha, tumeshafanyia kazi mapungufu yote na mengine benchi la Ufundi linaendelea kuyafanyia kazi ili Jumamosi tuwe tayari kukabiliana na Coastal,” amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: