Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Bado tuna imani na wachezji wetu

Amri Kiemba Ataja Kilichowaponza Simba Hadi Kushushiwa Kichapo Simba: Bado tuna imani na wachezji wetu

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klanbu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kejeli licha ya kufungwa na watani zao bao 5-1 kisha sare na Namungo FC kwa bao 1-1, bado wana imani na wachezaji wao.

Ahmed amesema hayo leo Novemba 16, 2023 wakati akizindua kampenzi ya hamasa kuelekea mchezo wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Novemba 25, 2023 katika Dimba la Mkapa.

“Sisi tuko bega kwa bega na wao, lakini tuwakumbushe kwamba yale yote yaliyopita wanapaswa waachane nayo, wasiingie uwanjani wakijihisi wakosefu au wanyonge kwamba tumewapelekea matatizo, waingie uwanjani kifua mbele kuipigania klabu yetu.

“Tuna imani na wachezaji wetu kwamba wanaweza kufanya makubwa na wameshathibitisha hilo, Novemba 25 wakaendeleze hayo makubwa. Tumeteleza hatujaanguka," amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: