Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Asec hazichekani hapa

Simba Vs ASEC Dar Simba, Asec hazichekani hapa

Sat, 9 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ikiwa Ligi ya Mabingwa Afrika imefika hatua ya robo fainali, kama kawaida timu nane zimefuzu baadhi zikiwa zimeonyesha viwango bora kwenye hatua ya makundi zikishika nafasi ya kwanza.

Hata hivyo, wakati vigogo hao wanaonekana kuwa na mwenendo mzuri kwenye michuano ya kimataifa tu, na mambo si mambo kwenye ligi za ndani.

Timu ya kwanza ambayo haifanyi vizuri kwenye ligi ni Asec Mimosas ya Ivory Coast iliyomaliza kundi B la Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa kinara ikikusanya pointi 11.

Katika Ligi Kuu Ivory Coast mambo sio mambo kwao, kwani inashika nafasi ya tano ikiwa na pointi 26 ilizokusanya kwenye mechi 15 ambapo imeshinda nane, sare mbili na kufungwa tano.

Timu inayoshika nafasi ya kwanza kwenye ligi hiyo ina pointi 34 ilizozipata kutokana na kucheza mechi 17, ambapo Asec ikishinda viporo vyake viwili ilivyo navyo itakuwa imepanda hadi nafasi ya pili ikiba na tofauti ya alama mbili na wanaoongoza.

Hata hivyo mchezo mmoja wa kiporo unaotarajiwa kuchezwa kesho unaonekana kuwa ngumu kwa sababu inacheza na Denguele inayoshika nafasi ya nne katika msimamo huo ikiwa na pointi zao 31 na imekuwa kwenye kiwango bora msimu huu.

Timu nyingine inayoonekana kutokuwa na mwenendo mzuri kwenye ligi ya ndani ni Simba ambayo inashika nafasi ya tatu ikikusanya alama 36 hadi leo jioni.

Licha ya kuwa na viporo vya mechi nne, hata hivyo ikiwa itashinda vyote itafikisha alama 48 ambazo hazitafikia pointi ambazo Yanga inayoongoza ligi ilizokusanya, ambayo nayo ikiwa itashinda mechi zake tatu za viporo itafikisha pointi 55.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: