Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Ahly timu ngumu, tutapambana nao

Simba Full Squad .jpeg Kikosi cha Simba

Wed, 11 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Klabu ya Simba imesema inakwenda kucheza mchezo mgumu dhidi ya Al Ahly ya Misri ambao ni mabingwa wa Afrika, lakini watapambana nao.

Hayo yamesemwa na Msemaji wa Simba, Ahmed Ally leo akieleza kuwa timu yao inakwenda kukutana na timu bora Afrika yenye rekodi kubwa.

Ally amesema Simba inatamani kuwa kwenye daraja ambalo Ahly wapo kwa sasa akiwataka mashabiki wao pia kujiandaa vyema kabla ya mchezo huo.

"Tunakwenda kukutana na timu ambayo imetuzidi kila kitu, hii ni klabu kubwa Afrika ina rekodi za kutosha ambazo sisi tunazitafuta,"amesema Ally

"Al Ahly wanashika namba moja kwa ubora wa Afrika na sisi Simba tunatamani kufika huko, mtaona jinsi ambavyo haitakuwa rahisi tunatakiwa kujiandaa na kupambana.

Hata hivyo, Ally amewataka mashabiki wa Simba kujindaa kwa umoja kuweza kumfunga bingwa huyo wa Afrika kwenye mchezo wa African Football League utakaopigwa Oktoba 20 pale Benjamin Mkapa.

"Hatutaweza kuwafunga Al Ahly kama hatutakuwa wamoja kuanzia mashabiki wetu, viongozi na timu yetu, kazi yetu ni moja tunatakiwa kuja kwa wingi kuishangilia timu kwenye mchezo huo."

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: