Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sikia mkwara wa Simba kwa ASEC Mimosas

Ahmed Ally Press Leo.jpeg Sikia mkwara wa Simba kwa ASEC Mimosas

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa kazi yao kubwa ni kupata ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas.

Mchezo huo wa hatua ya makundi unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Novemba 25 2023.

“Tunakazi moja tu ya kumnyoa ASEC Mimosas, tunatambua wapinzani wetu wataleta ushindani lakini tutapambana kufanya vizuri.

“Kikubwa Wanasimba wajitokeze kwa wingi kwenye mchezo wetu muhimu kwa kuwa wao ni muhimu kuongeza nguvu kwa wachezaji kupambana na kupata matokeo mazuri.

“Tupo nyumbani na huu ni mchezo muhimu kwetu kuanza safari ya kuyafuata malengo yetu mashabiki tuzidi kuwa pamoja a kushirikiana kama ambavyo sera yetu ya nguvu moja inasema,”.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: