Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sidi Bouna Amar, mashine Simba iliyoporwa na Waarabu

Sidi Bouna Amar Sidi Bouna Amar

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wydad Casablanca imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Sidi Bouna Amar akitokea Klabu ya Nouadhibou ya Mauritania utakaomuweka katika timu hiyo miaka mitatu, akiitosa Simba ambayo ilikuwa inanyemelea saini yake.

Simba ilikuwa inamfuatilia Amar kwa muda sasa ikimuweka kiporo, ikipiga hesabu za kwenda kumchukua mwisho wa msimu huu kabla ya Wydad kuingilia kati na kumsomba haraka.

Amar alikuwa miongoni mwa mastaa watatu wa Mauritania ambao kamati maalumu ya kusaka vipaji ya Simba ilimnasa na kuanza kufanya naye mazungumzo ya kumsajili.

Kasi yake akicheza kama winga ni moja ya ubora ambao anao Amar, ambapo kuanzia alipong'ara na kikosi cha Mauritania kilichoshiriki fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2022, zilizofanyika nchini Algeria jamaa alijizolea umaarufu mkubwa.

Amar anajua kufunga pia mbali na kukimbiza na kuwatoka mabeki akiwa pia na faida ya kucheza kama mshambuliaji feki, ambapo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika mpaka inasimama alikuwa na bao moja alilowafungia Pyramids ya Misri wakati Nouadhibou ikiwachapa Waarabu hao kwa mabao 2-0.

Akiwa na Mauritania kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zinazoendelea nchini Ivory Coast nako ana bao moja alilowafunga Angola wakati taifa lake likipokea kipigo cha mabao 3-2.

Hata hivyo, Wydad haitaweza kumtumia Amar kwenye mashindano ya Afrika kwa msimu huu akiwa tayari alikuwa ameshasajiliwa na Nouadhibou ambayo ipo kwwenye hatua hiyo, sababu ambayo pia Simba ilirudi nyuma kumalizana naye ikihofia hataweza kuwapa faida kubwa kwa sasa.

Wydad inaweza kumtumia Amar kwa ligi ya ndani pekee wakati huu ikipambana kurudisha ufalme wake baada ya kuwa na kikosi dhaifu kilichokuwa kinapoteza mechi nyingi kirahisi.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: