Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shomari Kapombe awajibu wanaombeza

Kapombe Simba G Shomari Kapombe awajibu wanaombeza

Thu, 28 Sep 2023 Chanzo: Dar24

Beki Kulia wa kikosi cha Simba SC, Shomari Kapombe, amesema siri ya ubora wake uwanjani ni nidhamu na kujituma.

Kapombe ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ndani ya kikosi cha Simba SC ambapo katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, ametengeneza pasi moja ya bao, akicheza mechi tatu, akikomba dakika 252.

Beki huyo amesema: “Kila kitu kinahitaji nidhamu hata uwanjani pia nidhamu inahitajika na kujituma kwa juhudi ili kufikia malengo ambayo tunahitaji. Mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kazi bado inaendelea.”

Jumapili (Oktoba Mosi), Simba SC inatarajiwa kumenyana na Power Dynamos ya Zambia kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, Uwanja wa Azam Complex, Dar, huku Kapombe akitarajiwa kuwa sehemu ya kikosi hicho.

Chanzo: Dar24
Related Articles: