Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shangazi afunguka sababu ya kujiuzulu Simba SC

Shangaziiiiiii Rashid Abdallah Shangazi

Fri, 7 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mbunge wa Jimbo la Mlalo na mjumbe kamati ya bodi ya wawekezaji wa Simba kupitia upande wa mwekezaji Mohamed Dewji, Rashid Abdallah Shangazi ameeleza sababu ya kujiuzulu kwake kwenye nafasi hiyo.

Shangazi amesema kuwa ameamuandikia Mohamed Dewji, barua ya kumuomba kujiondoa kwenye bodi ya uwekezaji tangu Juni 2 mwaka huu hii ni kutokana na mwenendo mbaya wa timu ya Simba.

"Kati ya mambo yaliyonifanya nijiuzulu ni kupisha mwekezaji kutengeneza safu mpya ya bodi itakayoisaidia klabu yetu kwani hatukuwa na matokeo mazuri kwa kipindi cha misimu miwili hivyo nimefanya hivi kama sehemu ya uwajibikaji," amesema Shangazi.

Amesema kuwa mwenendo mbaya wa timu yao umemfanya kupisha mwekezaji kutafuta watu wengine watakaoifikisha timu sehemu nzuri kama awali.

Shangazi amewataka wanachama na mashabiki kwa kuwa karibu zaidi na uongozi haswa katika kipindi hiki cha mapito.

"Uongozi ni kupokezana na unahitaji mshikamno na nguvu ya pamoja, msiiaache timu, sisi tumewajibika ili tujipange upya na tutaendelea kutoa michango yetu kadri itakavyohitajika," amesema Shangazi.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: