Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shaffih Dauda: Siamini kama Kocha wa makipa alitaka Aishi acheze jana

Shaffih Dauda Xtra Shaffih Dauda: Siamini kama Kocha wa makipa alitaka Aishi acheze jana

Mon, 6 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya mchezo wa jana kumalizika yangu ni haya nikianza na eneo la uchaguzi wa kikosi !

Kabla timu haijafikia uamuzi wa kupanga kikosi siku hizi ni tofauti na soka letu lilipotoka, siku hizi mtu ambaye anaamua nani acheze ni performance analyst hii ni kutokana na ripoti ya wiki nzima.

Yupo pia kocha wa magolikipa na wataalamu wa idara zingine, Kila mmoja atatoa ripoti kwa Kocha na wataishia hapo kwa sababu wao sio watoa maamuzi ya mwisho nani aanze kwenye kikosi

Mwalimu [Kocha Mkuu] ndio ataamua apange kwa kuangalia ripoti au apange kwa utashi wake mwenyewe lakini muda huo anakuwa tayari amepewa ripoti kutoka kwa wataalamu .

Mimi kama Shaffih Dauda siamini kwamba kocha wa makipa alimpitisha Aishi Manula akae golini jana yeye kama mtaalamu wa lile eneo!

Sitaki kuamini kwa profile ya ile game na ukiangalia Aishi amekaa nje ya uwanja kwa muda mrefu sioni kama hii mechi ilikuwa ni mechi sahihi ya yeye kucheza.

Huo ni msimamo na mtazamo wangu, Unaruhusiwa na wewe kuwa na mtazamo kwa sababu mpira ni mchezo wa wazi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: